SAMIA awapa Maagizo Haya Machifu wa Tanzania

0:00

10 / 100

Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza Machifu kutoka mikoa yote nchini kwenda kusimamia falsafa ya R4 katika utekelezaji wa majukumu yao ili kujenga misingi ya usawa, utawala bora, uwazi na uwajibikaji katika jamii wanazotoka.

Rais Samia ametoa maagizo hayo Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma leo alipokutana na Machifu hao na kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kuona namna gani jamii inaishi kwenye mila na desturi ya mtanzania ambayo kwa sasa inaonekana kutoweka.

“Tunaposema hakuna mtu aliye juu ya sheria, vivyo hivyo hakuna taasisi iliyo juu ya sheria mama ambayo ni Katiba yetu ya nchi. Katiba yetu inahimiza misingi ya usawa, utawala bora, uwazi na uwajibikaji. Mambo haya kwa ujumla yanasimamia haki ya mwanadamu. Hivyo basi ni wajibu wetu Machifu kuendesha kazi zetu kuendana na misingi ya Katiba na kusimamia haki kwa binadamu wote huku tukizingatia mila na desturi zetu.” Alisema Rais Samia.

Jambo jingine la tatu ambalo Rais Samia amelisisitiza kwa Machifu hao ni kuhakikisha mila, desturi na utamaduni wa mtanzania vinafuatwa katika jamii licha ya uwepo wa mabadiliko ya kidunia ambayo yanawafanya wanadamu pia kubadilika.

“Suala la nne ni kukuza utawala wa kidemokrasia na uwazi katika maeneo yetu kule. Kuna mambo mengi yanatokea Machifu mko huko chini, unakwenda pahali unakuta kuna malalamiko mengi ya wananchi, akitokea kiongozi wa chama au wa Serikali ndio wananchi wanakimbilia. Kuna mambo mengi huko yanatokea, tunaomba machifu tusaidieni, nyinyi kama viongozi wa jamii mliokubalika kule, migogoro mingine hii tusaidieni.” Aliendelea Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amewaagiza Machifu hao kwenda kutoa elimu kwa viongozi wa kisiasa katika maeneo wanapotoka kuhusu kuondokana na dhana ya imani za kishirikina inayosababisha kufanyika kwa vitendo vya kikatili katika jamii.

See also  DIANE RWIGARA AMNYOOSHEA PAUL KAGAME KIDOLE

Rais Samia amekutana na Machifu hao ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa Septemba 8, 2021 katika Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania lililofanyika wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

ALIYEUWA NDUGU WAWILI KUNYONGWA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA HIVI LEO 09/07/2024
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Police Apologize for Mistaken Arrest of Veteran...
The National Police Service (NPS) has described the forceful arrest...
Read more
SABABU MARIOO KUFUNGULIWA KESI
NYOTA WETU Msanii Toto Bad maarufu kama @marioo_tz amefunguliwa kesi...
Read more
Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain...
Inaelezwa kuwa, mabosi wa PSG wanataka kumchukua fundi huyu ikiwa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply