Dodoma.
Rais wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan amewaapisha MabaloziWateule Ikulu Chamwino Dodoma leo Agosti 16,2023 ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba ni kwamba kuna Mabalozi ni kama vile hawajui wanachokifanya kwakuwa wapowapo tu na hawafanyi kazi kwa ufanisi.
“Katika Nchi nyingine Mabalozi wetu sijui niseme hawajui wanachofanya ,wapo tu,nilishakutana na Rais mwenzangu ndani ya Nchi za Afrika, ndani ya SADC akaniambia nibadilishe Balozi ulieniletea hata kazini haendi, mikutano hashiriki yupoyupo tu hatuelewi ,Tanzania hatujawazoea hivyo sasa labda ubadilishe nikamwambia nimekusikia”
“Lakini Mabalozi wengine unawaona pale ambapo Ujumbe wa Tanzania umekwenda kwenye Nchi hiyo ,au siku za kisherehe za kitaifa za Nchi hiyo anakwenda kuwakilisha Nchi yake lakini mengine hakuna ,au labda Watanzania wafanye ukorofi wakamatwe huko utaona taarifa ya Balozi Lakini vingine huoni”
“Sasa inawezekana pia labda na aina ya Mabalozi tunaowapeleka inawezekana ,karibuni hivi nilitengeneza kamati ipitie Wizara hii ya Mambo ya Nje niletee kasoro zilizopo ,nimepokea draft ya kwanza nimewarudishia wanaendelea kuifanyia kazi nadhani ripoti itakapokuja itasaidia turekebishe Wizara yetu”.
Baada ya kauli hizi za Mheshimiwa Rais ,Mhariri wetu alijilidhisha kuwa yote kwa yote ,Balozi Emanuel Nchimbi ndiye Alikuwa mlengwa hapa.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.