EVERTON YAPATA MMILIKI MPYA

0:00

Michezo

Kampuni ya Uwekezaji kutoka Marekani imefikia makubaliano ya kununua asilimia 94.1 ya hisa za klabu ya Everton kutoka kwa aliyekuwa mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshiri.

Farhad Moshiri

Kukamilika kwa dili hilo kunategemea idhini maalum kutoka kwa shirikisho la soka England (FA) ,hivyo utimilifu wake utaifanya Everton kuwa sehemu ya klabu zinamilikiwa na taasisi ya 777 ,ambayo pia inamiliki klabu kama Sevilla,Genoa,Hertha Berlin pamoja na Standard Liege ya Ubelgiji.

Licha ya aliyekuwa mmiliki wa klabu hiyo, Farhad Moshiri kuwekeza zaidi ya pauni milioni 750 tangu 2016,baadhi ya mashabiki wa Everton wamekuwa wakiupinga vikali utawala wa Moshiri ,kwa kufanya maandamano yaliyoshinikiza kung’atuka kwake.

Everton imedhamiria kupambana na kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja baada ya kuanza kusuasua huku kikosi cha Sean Dyche kikishika nafasi ya 18 kikiwa kimevuna alama moja pekee katika michezo minne ya Ligi ya EPL mpaka sasa.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

JEFF BEZOS MTU TAJIRI ZAIDI DUNIANI AMBWAGA...
MAKALA BILIONEA Jeff Bezos amerejea kwenye usukani wa ukwasi Duniani baada...
Read more
JOSE MOURINHO AMPA ONYO MIKEL ARTETA
MICHEZO Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Chelsea na Man Utd...
Read more
WAYS ON HOW TO SHOW TRUE LOVE...
LOVE TIPS ❤ 12 WAYS ON HOW TO SHOW YOUR...
Read more
MTANZANIA MWINGINE AUAWA KWENYE MAPIGANO ISRAEL ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
WHY A CHEATING WOMAN IS MORE DANGEROUS...
A CHEATING WOMAN IS MORE DANGEROUS THAN POISON A man can...
Read more
See also  MFAHAMU MLINZI BINAFSI WA LEO MESSI

Leave a Reply