TUNDU LISSU akerwa na uhusiano wa Mbowe na Serikali

0:00

4 / 100

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu , ameweka wazi sababu za kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa na kutoa maoni yake kuhusu changamoto za kisiasa nchini.

Lissu ameyasema hayo wakati wa mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha habari cha Voice of America (VOA), ambapo amezungumzia masuala ya mabadiliko ndani ya chama na hatua za kulazimisha mageuzi ya kidemokrasia nchini.

Lissu amesema CHADEMA inahitaji uongozi mpya ambao utaiondoa nchi kutoka kwenye mkwamo wa kisiasa uliopo sasa. Ameeleza kuwa mazungumzo ya maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo yamefanyika kwa takriban miaka miwili hayajazaa matunda yoyote, akisisitiza kuwa ni wakati wa kuanzisha “Nguvu ya Umma” (mass mobilization) ili kuamsha taifa na kushirikiana na asasi za kiraia na vyama vingine vya siasa kulazimisha mabadiliko ya kidemokrasia.

“Tunatakiwa kufanikisha mabadiliko makubwa ya kidemokrasia ili kulazimisha mabadiliko ya mfumo wa uongozi,” amesema Lissu.

Alipoulizwa kuhusu tofauti kati yake na Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA, Freeman Mbowe , Lissu amekiri kuwa kuna tofauti za kimsingi juu ya namna ya kukipeleka chama mbele. Amedai kuwa uongozi wa sasa haujachukua hatua za kutosha kupambana na changamoto zinazolikabili taifa, kama vile utekaji na mauaji ya wanachama wa chama hicho.

“Chama kinaonekana kipo nusu kaputi kwa sababu Mwenyekiti haonekani kutaka kubomoa daraja na uongozi wa Rais Samia,” amesema Lissu.

Lissu ameeleza msimamo wa CHADEMA kuhusu kushiriki uchaguzi, akisema chama hicho hakitashiriki chaguzi zozote zijazo kama hakutakuwa na mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi. Amerejelea uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, na mitaa uliofanyika hivi karibuni, akisema ulikuwa “majanga” kwa kiwango cha udanganyifu kilichofanywa.

See also  "KUKOPA NI AFYA KWA UCHUMI " GEORGE SIMBACHAWENE

“Tumesimama kwenye msimamo wa No Reforms, No Election. Lazima tupiganie mabadiliko kabla ya kushiriki chaguzi,” amesisitiza Lissu.

Lissu ametoa wito wa mabadiliko ndani ya CHADEMA, akisema chama hicho hakiwezi kupambana na changamoto za nje kama hakitasafisha mfumo wake wa ndani. Amependekeza kuwepo kwa ukomo wa uongozi na kuweka mifumo inayohakikisha uwazi na uwajibikaji ndani ya chama.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kamala Harris acknowledged Donald Trump’s victory in...
In a significant turn of events, Kamala Harris has officially...
Read more
BASSIROU DIOMAYE FAYE AAPISHWA RASMI KUWA RAIS...
NYOTA WETU Mwanasiasa wa mrengo wa kushoto, Bassirou Diomaye Faye,...
Read more
TABIA 10 ZINAZOFANYA WANANDOA KUISHI KWENYE NDOA...
MAPENZI Kuzeeshana kwenye ndoa ni jambo ambalo kila mwanandoa analitamani...
Read more
DARAJA LA FRANCIS SCOTT KEY LAUA WATU...
HABARI KUU Sita wahofiwa kufa tukio la daraja kuporomoka Marekani Huku...
Read more
WHY I WANT TO VISIT VERYDARKMAN IN...
OUR STAR 🌟 The aphrodisiac businesswoman, Jaruma Empire weighs in on...
Read more

Leave a Reply