Ni Kanisa Katoliki au Padri Kitima,CHADEMA?

4 / 100

Wakati vuguvugu la siasa likiendelea kutikisa nchi, mvutano baina ya wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Tundu Lissu unaendelea kuwa mkali.

Lakini moja ya taarifa zinashtua ni ile inayomhusisha Padri Charles Kitima, Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC), katika juhudi za upatanishi wa wanasiasa hao zinazodaiwa kufanyika kwa siri.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, na kauli zilizotolewa na mwanasiasa Tundu Lissu akiwa uwanja wa ndege, vikao hivyo vilikuwa vikifanyika usiku. Uchunguzi wetu umebaini kuwa vikao hivyo havikuwa rasmi kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Katoliki, bali ilikuwa ni juhudi binafsi za Padri Kitima. Lissu alibainisha kuwa mada kuu za vikao hivyo zilihusu nani atagombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na nani atagombea urais.

Imeelezwa kuwa Padri Kitima ndiye aliyeitisha vikao hivyo; akipanga tarehe na muda na kisha kuwapigia simu washiriki ambao walikua ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Makamu wake Tundu Lissu na Katibu Mkuu John Mnyika kwa lengo la kufanya maamuzi ya nani awe Mwenyekiti wa chama, na nani awe mgombea Urais wa chama katika uchaguzi utakaoanza Julai 2025.

Swali kubwa linabaki: Padri Kitima ana nafasi gani ndani ya CHADEMA kiasi cha kushiriki moja kwa moja kwenye maamuzi makubwa ya chama? Je, hili linaweza kuchukuliwa kama upatanishi wa kiroho au kuna taswira nyingine inayoonekana?

Taarifa zingine zinadai imekua ni kawaida kwa Padri Kitima kufanya vikao vya kimkakati na viongozi na CHADEMA, na imekua ni bahati mbaya tu taarifa za vikao vya safari hii kuvuja baada ya Tundu Lissu kueleza wazi wakati akijibu maswali ya wanahabari.

See also  KWANINI PAUL KAGAME ANAMHOFIA DIANE RWIGARA?

Hisia mseto zimeibuka miongoni mwa watu. Wapo wanaoona hatua hii kama ya kiungwana, ikizingatiwa nafasi yake kama kiongozi wa kiroho, lakini wapo pia wanaohisi kuwa kuna mahusiano ya karibu yasiyoeleweka msingi wake wala mipaka yake baina ya Padri Kitima na chama cha CHADEMA.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

Undefeated PSG ease 3-0 past Toulouse
PARIS,- Leaders Paris St Germain beat Toulouse 3-0 in Ligue...
Read more
BBNaija officially revealed the start date for...
The official launch date for the highly anticipated season 9...
Read more
Wolfsburg dump Dortmund out of German Cup...
WOLFSBURG, Germany, 🇩🇪 - Jonas Wind struck late in the...
Read more

Leave a Reply