Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Diwani Kata Mwembesongo Mhe.Ally Rashidi Kalungwana Kwa kitendo cha Kutumia vibaya madaraka yake kujenga vibanda vya biashara katika eneo la wazi Soko Kuu la chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro

0:00

DC Rebbeca amesema Diwani huyo amejenga vibanda vya kufanyia biashara katika Soko Kuu la Chifu Kingalu bila kufuata taratibu za mipango miji jambo ambalo ni kosa kisheria na kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu haraka sana Ili iwe fundisho kwa watu wengine.

DC Rebbeca anasema licha ya Diwani huyo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mipango miji Halmashauri Manispaa ya Morogoro, lakini amekua mtu wa kwanza kuvunja sheria hivyo lazima awe mfano kwa watu wanaotumia madaraka yao vibaya.

Mwenyekiti wa soko Hilo la Chifu Kingalu, Khalid Mkunyegele anasema licha ya uongozi wa soko kumkataza kujenga lakini alikaidi amri hiyo na kuendelea hadi kamati ya usalama Wilaya ilipofika na kubomoa vibanda hivyo ambayo vimejengwa pembeni ya soko kuu .

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Gharama Halisi za Kupata Leseni ya Kutengeneza...
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kanuni zake za sasa...
Read more
WHY YOU SHOULD CREDIT YOUR MAN THIS...
OUR STAR 🌟 Famous singer, Patoranking reveals why ladies ought...
Read more
COMMON MONEY MISTAKES TO AVOID
BUSINESS 10 common money mistakes to avoid Mistake 1 Not...
Read more
Environment CS Nominee Declares Corruption Greater Threat...
Aden Duale, the nominated Environment Cabinet Secretary of Kenya, has...
Read more
Kwanini Rais Kim Jong-un Hawezi Kushambuliwa kama...
Kwanini Kilichomfika Trump Ni Vigumu Kumfika Komredi Kim Jong Un..? Jibu: Dunia...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  MACKY SALL KUONDOKA MADARAKANI

Leave a Reply