CHAKULA CHA WAMAREKANI KIKO SALAMA YASEMA TBS

0:00

HABARI KUU

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema msaada wa chakula uliotolewa na wizara ya Kilimo ya Marekani kwa ushirikiano na Taasisi za Jumuiya ya Kimataifa katika baadhi ya shule za mkoa wa Dodoma ulifuata taratibu za uingizwaji wa chakula nchini.

Taarifa ya TBS iliyotolewa kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa chakula hicho kilipoingizwa nchini kilifanyiwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi.

TBS imetoa taarifa hiyo kufuatia taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na msaada wa mchele ulioongezwa virutubishi, mafuta ya kupikia yaliyoongezwa virutubishi na maharage vilivyotolewa na taasisi hizo za nchini Marekani kupitia mpango wa Pamoja Tuwalishe.

Aidha, TBS imesisitiza kuwa utaratibu wa kuongeza virutubishi kwenye chakula unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MWALIMU ALIYETOA ADHABU YA KUZIBUA VYOO HATIANI
HABARI KUU Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani...
Read more
HOW YOU CAN SUCCESSFULLY RAISE BROILER CHICKENS?
You are a beginner in poultry entrepreneurship, let's look at...
Read more
SEAN COMBS HAS BEEN ACCUSED BY A...
Rapper and businessman Sean Combs "Diddy", has been accused by...
Read more
MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA 24,2023 ...
Magazeti Karibu Mtanzania, asubuhi hii ya leo uone kilichojiri kwenye...
Read more
3 THINGS YOU NEED TO DO TO...
1) HAVE STANDARDS From dozens of practical counseling sessions I've done...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Kwanini Mchezaji Roberto Firmino Amegeukia Kazi ya Injili?

Leave a Reply