NYOTA WETU
Meneja wa zamani wa timu ya Taifa ya England Sven-Goran Eriksson (76) alitokwa na machozi jana alipofanikiwa kutimiza ndoto yake kuu ya kabla ya kifo.
Januari mwaka jana Kocha huyo mkongwe alitangaza kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ambao uko kwenye hatua za mwisho na hivyo siku zake za kuishi si nyingi.
Katika mahojiano na Shirika la habari la Sky News mwaka jana Eriksson alisema ndoto yake kubwa ambayo hakufanikiwa kuitimiza ni kuwa Meneja wa Liverpool.
Jumamosi ya jana ndoto hiyo ilitimia kwani alipewa nafasi ya kusimamia mechi ya hisani ya wakongwe kati ya Liverpool na Ajax iliyochezwa huko Anfield.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mechi, Eriksson alisema “kukaa kwenye benchi la Liverpool ilikuwa ndoto yangu kubwa, leo imetimia, imekuwa siku nzuri, na kumbukumbu njema sana”.