MICHEZO
Related Content
Related Content
Wachezaji wa Yanga SC viungo Khalid Aucho, Pacome Zouazoua na mlinzi Yao Attohoula ni miongoni mwa
wachezaji wa Yanga SC waliosafiri na kikosi hicho kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya pambano la marudiano dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Nyota hao walilikosa pambano la kwanza lililofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kutokana na kuwa na majeraha.
Kitendo cha nyota hao kuongozana na kikosi hicho katika mchezo huo kinatoa tafsiri kuwa huenda wakawa sehemu ya kikosi kitakachoanza katika pambano hilo la marudiano.
Mchezo huo wa kwanza ulimalizika kwa sare tasa na Yanga SC wanahitaji ushindi au sare ya mabao waweze kufuzu hatua ya nusu fainali.
