KIKOSI CHA SIMBA KILIVYOWASILI CAIRO MISRI USIPIME

0:00

MICHEZO

Kikosi cha Simba SC kimewasili salama mjini Cairo, Misri tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Pili wa Robo Fainali, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Mabingwa watetezi Al Ahly.

Simba SC itacheza mchezo huo keshokutwa Ijumaa (Aprili 05) katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, ikiwa na deni la kulipa bao 1-0, baada ya kupoteza mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Ijumaa (Machi 29).

Kikosi cha Simba SC kilianza safari mapema leo Jumatano (Aprili 03), kikiwa na wachezaji 23, viongozi wa Benchi la Ufundi na viongozi wa klabu pamoja na mashabiki 17 ambao wamejilipia gharama zao wenyewe.

Orodha ya wachezaji iliyotolewa na Simba SC Walinda Lango ni Ayoub Lakred, Ally Salim na Hussein Abel.

Mabeki: Shomari Kapombe, Israel Mwenda, David Kameta ‘Duchu’, Mohamed Hussein, Henock Inonga, Che Fondoh Malone, Kennedy Juma na Hussein Kazi.

Viungo: Babacar Sar, Sadio Kanoute, Fabrice Ngoma, Mzamiru Yassin, Abdallah Hamisi, Saido Ntibazonkiza, Kibu Denis, Luis Miquissone, Clatous Chama na Essomba Onana.

Washambuliaji: Pa Omar Jobe na Freddy Michael.

Katika mchezo huo hiyo, Simba SC inahitaji ushindi wowote wa kuanzia mabao mawili ili kusonga mbele

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MotoGP bikes to use same engines in...
Motorcycle manufacturers will have to use their 2025 engines in...
Read more
Manchester United part-owner Sir Jim Ratcliffe is...
Ratcliffe's arrival at the club was ratified shortly after the...
Read more
7 BODY PARTS YOU SHOULD NEVER IGNORE...
THREAD1. The neck The neck is the body’s most vulnerable zone....
Read more
ILIKUWA NDOTO SASA IMEKUWA KWELI ...
Magazeti
See also  Suna East Residents Demand Urgent Road Repairs
Ni Septemba 28,2023 karibu Mtanzania kwenye mbao za magazeti...
Read more
Singer Fireboy addressed the buzz surrounding his...
Nigerian music sensation Adedamola Adefolahan, widely recognized as Fireboy, has...
Read more

Leave a Reply