SIASA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Nyasa ambaye pia anagombea kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho, Mchungaji Peter Msigwa amewasilisha malalamiko dhidi ya Mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho John Mrema kwa kile alichokitaja kuwa mgongano wa masilahi katika uchaguzi wa kanda wa chama.

Katika barua aliyomwandikia Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, Msigwa ameeleza kuwa mwenendo wa John Mrema unazua maswali kwani ameonesha...