Zurich
Shirikisho la soka Duniani, FIFA,linapanga kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya Rais wa Shirikisho la soka nchini Uhispania ,Luis Rubiales, kutokana na kitendo alichokionesha wakati wa fainali ya kombe la Dunia la Wanawake siku ya Jumapili.
Rais huyo alimbusu mchezaji wa Timu ya Taifa ya Uhispania, Jenni Hermoso ,mdomoni wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi, mara tu baada ya Uhispania kuishinda Uingereza.
FIFA itafanya uchunguzi hili kubaini iwapo vitendo hivyo vinakiuka kifungu cha 13 cha kanuni za nidhamu ,ambacho kinalenga tabia yenye kuudhi na uchezaji wa haki.
Kanuni inasema, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya yeyote anayekiuka “kanuni za msingi za tabia njema”kumkosea heshima mtu au mwanasheria kwa njia yoyote haswa kwa kutumia ishara au lugha yenye kudhalilisha au “kuonyesha tabia yenye kuharibu sifa ya mchezo wa mpira wa miguu au #FIFA”