Dar es salaam.
Ligi ya NBC TANZANIA imeendelea leo kwa mchezo mmoja uliovurumshwa kwenye dimba la Chamanzi ukiwakutanisha Young Africans na Maafande wa JKT. Mchezo huu umeanza kwa timu zote mbili kucheza kwa tahadhali kubwa huku maafade wa JKT wakionekana kuwamiliki vizuri vijana wa Yanga.
#Yanga inayonolewa na Muargentina Gamondi imefanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya “45”+”5″ kupitia kwa mkwaju wa kutenga mita chache kwenye lango la JKT,mkwanju huo umefungwa na Aziz Ki. Baada ya goli hilo timu ziliingia mapumziko huku ikionekana mchezo huko hamsini kwa hamsini.
Yanga walirudi kama Mbongo ambapo alikuwa ni Msonda dakika ya 54 alipokwamisha pasi safi ya Max Nzengeli ,kabla ya Yao kukwamisha mpira wake kwa shuti la mbali lililomshinda kipa wa JKT TANZANIA mnamo dakika ya 64. Nae nyota wa mchezo wa leo Max Nzengeli amehitimisha kalamu ya mabao matano kwa kufunga magoli dakika za 79 na 87.
Mpaka sasa Yanga inakaa kileleni mwa ligi ya NBC Tanzania kwa kujikusanyia magoli 10 bila kuruhusu nyavu zao kuguswa katika michezo miwili iliopita ya KMC na JKT.