FAIDA 6 ZA KUFANYA MAPENZI ASUBUHI

0

0:00

MAPENZI

Angalizo ni kwamba hii ni maalumu kwa waliopo kwenye ndoa lakini pia na wanandoa watarajiwa.

1. KUFANYA MAPENZI ASUBUHI NI MOJA YA MUDA MZURI KULIKO MUDA MWINGINE WOWOTE.

Kuna amsha hali ya kuingia kwenye uwajibikaji wa kazi zako .” Cha asubuhi ” ni dawa ya kuondoa wasiwasi , kupunguza misuli kukaza,uongeza uwezo wa kuzaliana, pia inakupa uso mg’avu na sura ya matumaini.

2. UPUNGUZA WASIWASI AU KUTOKUJIAMINI.

Unapofungua macho asubuhi na kuanza kuwaza siku itakavyokuwa na ukatishika basi “cha asubuhi ” ndio dawa. Ubongo huwa unapunguza ukubwa wa msongo kutokana na tendo lenyewe . Raha ya tendo hufanya homoni ya Endorphin inayohusika na suala la hisia nzuri na furaha kuzalishwa zaidi. Inatajwa homoni ya Endorphin ina kazi ya kuondoa msongo,kuamsha hali na kupunguza maumivu ya mwili.

3. NI MOJA YA MAZOEZI MAZURI.

Kama ni mtu wa kuamkia sehemu kama za Gym au kukimbiza upepo,basi uzoefu unaonyesha kufanya mapenzi ni moja ya zoezi zuri na toshelevu. Kufanya mapenzi, ni zaidi ya zoezi hasa kwa wenye mafuta mengi maana huchoma kiasi kikubwa cha mafuta yasiyotakiwa mwilini (calories). Sasa wakati umefika, badala ya kuamuka na kukimbilia kwenye Gym,mkimbilie mwenza wako.

4. HUSAIDIA UWE NA MUONEKANO WA UJANA.

Kila mmoja wetu angependa awe na mwonekano wa ujana na mwenye siha njema , tiba ni kufanya tendo la ndoa. Homoni ya Estrogen inayozalishwa wakati wa umwagaji wa manii inasaidia uwe na mwonekano wa ujana na uwe mzuri pia. Husaidia ngozi kuwa laini na nyororo na kupunguza makunyanzi ya ngozi na sio pekee tu bali hata kwenye mzunguko wa damu.

5. HUJENGA UKARIBU.

Si unajua kufanya tendo la ndoa na mwenza wako huwa lina raha yake? Wakati wa tendo hili, kemikali ya Oxytocin huzalishwa na kazi ya kemikali hii ni ya kugeuza watu kuwa kitu kimoja. Hii ndio kemikali husababisha mama na mtoto kuwa na ukaribu na hata baada ya kuzaliwa ,ambayo huwa inazalishwa kwenye tendo la ndoa. Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa, Oxytocin ina mchango mkubwa wa kusababisha kuwepo na ndoa ya kuoa mke mmoja.

6. CHANZO CHA KUZALIANA.

Kama tujuavyo,mipango huanza asubuhi na hata kuamkia kwenye tendo la ndoa ni njia moja ya kufikia utungishaji wa mimba wa sahihi kwasababu ni mpango. Homoni za testosterone zipo kwa wingi asubuhi ambazo hufanya wanaume wengi kuamka wamesimamisha. Pia, cha asubuhi ni tiba ya kansa ya tezi dume na pia husaidia kupunguza maumivu ya kichwa.

Ungependa kufahamu “CHA ASUBUHI ” kinafanyika muda gani? Muda mzuri ni saa 10 usiku na baada ya hapo jipe muda wa kulala hata lisaa lingine moja kabla ya kuamka na kuendelea na shughuli zako za kila siku.

Mujuni Henry
See also  KILLERS OF MARRIAGE YOU HAVE TO KNOW
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading