SERIKALI YA NIGERIA YAFANIKIWA KUWARUDISHA MATEKA 137

0:00

HABARI KUU

Maafisa nchini Nigeria wamethibitisha kuokolewa kwa watu 137 waliotekwa na watu wenye silaha huko Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo wiki mbili zilizopita.

Taarifa zimeeleza kuwa operesheni ya uokoaji ilifanyika alfajiri ya leo ikiwa ni siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ya malipo yaliyoombwa na watekaji hao.

Gavana wa Jimbo la Kaduna Uba Sani amesema wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa shule wameokolewa kutokana na ujasiri wa maafisa wa usalama.

Wiki iliyopita majambazi hao walidai kiasi cha pauni 486,000 ili kuwaachia watu hao, hata hivyo Rais Bola Tinubu aliahidi kuwaokoa bila ya kulipa hata senti moja.

Idadi ya wanafunzi na wafanyakazi wa shule waliotekwa katika wiki za hivi karibuni ni 287 hivyo takribani nusu yao bado wanashikiliwa mateka.

Majambazi hao wamekuwa wakiwateka nyara maelfu ya watu katika miaka ya hivi karibuni nchini humo na kuwaachia huru mara baada ya kulipwa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MADHARA YA FANGASI UKENI NA TIBA YAKE
AFYA MADHARA YA FANGASI UKENI👇 Madhara yafuatayo yanaweza kutokea ikiwa mgonjwa mwenye...
Read more
NBA roundup: Luka Doncic powers Mavs past...
Luka Doncic had 32 points, nine rebounds and seven assists...
Read more
National women doubles pair Pearly Tan and...
The duo have booked their spot in the quarter-finals of...
Read more
The Premier League have officially announced the...
The Nike Flight Premier League ball will enjoy its first...
Read more
19 TRUTHS ABOUT SEX AS GOD'S GIFT...
LOVE ❤ 1. SEX IS GOD'S GIFT FOR MARRIAGE...Sex is...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  ANAYEDAI KULAWITIWA NA ALIYEKUWA RC SIMIYU AMUOMBA RAIS SAMIA KUINGILIA KATI SAKATA LAKE

Leave a Reply