MICHEZO
Imefahamika kuwa Kocha kutoka nchini Ureno Jose Mourinho anafahamu kila kitu kuhusu mpango wa kuhusishwa na ajira kwenye klabu ya SL Benfica.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Inter Milan anahusishwa na SL Benfica kwa ajili ya msimu ujao 2024/25, kufuatia kocha mkuu wa sasa wa klabu hiyo Roger Schmidt, kuhusishwa na Klabu ya Liverpool ya England.
Taarifa zinaeleza kuwa Mourinho alighairi ziara ya uwanjani ili asizue machafuko zaidi miongoni mwa mashabiki na waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia mchezo wa ligi kuu ya Ureno kati ya SL Benfica dhidi ya Moreirence iliyokubali kipigi cha mabao 3-0.
Mourinho alipanga kufanya hivyo kwa lengo la kupunguza chokochoko zinazoendelea dhidi yake za kuhamia kwenye klabu ya SL Benfica, hasa katika kipindi hiki ambacho hana ajira.
Kwa mara ya mwisho Mouronho alikuwa Kocha Mkuu wa AS Roma ya Italia, lakini alitimuliwa na klabu hiyo Januari 16 kufuatia mambo kumuendea kombo uwanjani.