Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekiri kuwa chama chake cha African National Congress (ANC) kimepata changamoto katika matokeo ya uchaguzi, baada ya chama hicho kupoteza wingi wa kura kwa mara ya kwanza tangu utawala wa kibaguzi kumalizika miaka 30 iliyopita.

0:00

10 / 100

Chama cha ANC, ambacho kiliwahi kuongozwa na Nelson Mandela, kilishinda viti 159 katika bunge lenye viti 400 katika uchaguzi wa Jumatano, idadi ya chini kutoka 230 katika bunge lililopita.

Ramaphosa bado alitaja matokeo kama ushindi kwa demokrasia, akitoa wito kwa vyama vinavyopingana kutafuta muafaka na kujiandaa kwa mazungumzo ya muungano.

Chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) kimesema kiko tayari kwa mazungumzo ya muungano na Bw Ramaphosa, lakini kinapinga vipaumbele vingi vya serikali yake.

Pamoja na kura zote kuhesabiwa, ANC ilimaliza kwa kupata 40% chini kutoka 58% katika matokeo ya uchaguzi uliopita, ambayo yalitangazwa siku ya Jumapili.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SITI BINTI SAAD: JOHARI LA MUZIKI WA...
Siti Binti Saad (1880 - 1950), alikuwa ni mwimbaji maarufu...
Read more
IPOA Condemns Acting IG Masengeli for Court...
The Independent Policing Oversight Authority (IPOA) has condemned the actions...
Read more
IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA NGARAMTONI ARUSHA...
HABARI KUU Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya barabarani...
Read more
GARI LA SHULE YA KEMEBOS LAUA MWANAFUNZI...
HABARI KUU Mwanafunzi wa kidato cha tano, Frank Matage kutoka...
Read more
MFAHAMU MLINZI BINAFSI WA LEO MESSI ...
Michezo Nyota wa Inter miami na mshindi mara 7 wa balloon'dor...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  MOHAMED DEWJI KUFANYA USAJILI MWENYEWE SIMBA

Leave a Reply