MWENYE SEHEMU ZA SIRI MBILI AONDOLEWA UKE

0:00

HABARI KUU

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke imefanyia upasuaji wa kutoa viungo vya uzazi vya kike (uke) kutoka kwenye korodani ya mgonjwa wa jinsia mbili mwenye mwonekano wa jinsia ya kiume ikiwa ni mara ya kwanza upasuaji huo kufanyika katika hospitali za rufaa zilizopo Tanzania.

Upasuaji huo umefanywa na jopo la Madaktari kutoka hospitali hiyo, na limeongozwa na daktari Bingwa wa upasuaji wa jumla na mfumo wa mkojo,Dkt Hussein Msuma pamoja na wasaidizi wake ,Dkt. Hamis Mbarouk ,Curtuis Mbalamula ,Mkati na Shani Maupa.

Taarifa ya hospitali hiyo imeeleza kuwa kufanyika kwa upasuaji huo ni moja ya mafanikio makubwa kwenye sekta ya afya Tanzania kwa kuwa moja ya jitihada za serikali na Wizara ya Afya kwa ujumla ni kuhakikisha hospitali zina uwezo wa kutoa matibabu ya kibingwa na Ubingwa bobezi.

Akizungumza baada ya upasuaji kufanyika na kufanya vipimo vya sampuli zilizotolewa katika upasuaji, Dkt Msuma amesema mgonjwa alifika hospitalini akiwa na mwonekano wa jinsia ya kiume lakini ana maumbile ya ndani ya aina mbili ,yaani maumbile ya kiume na kike ,hivyo kupelekea upasuaji huo.

“Alikuwa na mifumo ya uzazi ya jinsia mbili,ya kiume kwenye korodani ya kulia na ya kike kwenye korodani ya kushoto “

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Osimhen strike saves Nigeria in Abidjan
An 81st minute equaliser from Galatasaray forward Victor Osimhen laminated...
Read more
Martinez strike earns Inter 1-0 win over...
Inter Milan secured a 1-0 victory at AS Roma on...
Read more
RAINFORD KALABA AFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA...
NYOTA WETU
See also  MVUA YAKATISHA MAWASILIANO KATAVI NA KIGOMA
Kiungo mshambuliaji wa TP Mazembe na timu ya...
Read more
Serikali ya Tanzania Yashitakiwa Kwa Kuzima Internet
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshitakiwa kikatiba katika...
Read more
MAMBO 10 YA KUMWAMBIA MWANAMUME AJIONE MWENYE...
MAPENZI Siku zote,mwanaume anahitaji kupata heshima na anapoona anapata hicho...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply